Machi 4 watatangazwa watakatifu watatu wa kanisa - | vatican news

Play all audios:

Tarehe 4 Machi Papa Fancisko ataongoza Masifu ya Tatu na kufanya Mkutano wa kawaida na makardinali kwa ajili ya kuwatangaza watakatifu watatu:mwenyeheri Titus Brandsma,Kuhani mfiadini na wa
Shirika la Wakarmeli;Mwenyeheri Maria Rivier,Mwanzilishi wa Shirika la Watawa wa Kike wa Kumwakilisha Maria;Mwenyeheri Maria wa Yesu,Mwanzilishi wa Shirika wa watawa wa kike wakapuchini NA
ANGELLA RWEZAULA – VATICAN. Ofisi ya maadhimisho ya liturujia za kipapa imetoa taarifa kuwa tarehe 4 Machi 2022 utafanyika Mkutano (Consistory) wa kawaida wa umma na makardinali kwa ajili
ya kupitisha baadhi ya watakaotangazwa watakatifu saa 4.30 katika Ukumbi wa Mkutano kwenye Jumba la Kitume Vatican. Papa Fancisko katika siku hiyo ataongoza Masifu ya Tatu na Mkutano huo wa
kawaida wa umma na makardinali kwa ajili ya kuwatangaza watakatifu watatu wafuatao: mwenyeheri Titus Brandsma, Kuhani mfiadini na mwenye nadhiri wa Shirika la Wakarmeli; Mwenyeheri Maria
Rivier, Mwanzilishi wa Shirika la Watawa wa Kike wa Kumwakilisha Maria; Mwenyeheri Maria wa Yesu (zamani aliitwa Carolina Santocanale), Mwanzilishi wa Shirika wa watawa wa kike waKapuchini
wa Moyo safi wa Lourdes. Kwa maana hiyo Makardinali wanaoishi Roma na walioko Roma katika Siku hiyo ya Mkutano, wanaomba kukutana saa 4.00 kamili siku hiyo kwenye Ukumbi wa Mkutano wa Jumba
la Kitume wakiwa na mavazi tayari ya maadhimisho.