Wanawake katoliki duniani na Papa:Tumepeleka sauti zilizosahaulika!

Play all audios:

2022.06.11 UMOFC - MARIA LIA ZERVINO - MONICA SANTAMARINA Baba Mtakatifu Wanawake katoliki duniani na Papa:Tumepeleka sauti zilizosahaulika! Bi María Lía Zervino,Mwenyekiti wa Umoja wa
Vyama vya Wanawake Katoliki ulimwenguni amesimulia kuhusu Mkutano wa Baraza la Utendaji la kiungo cha wanawake na Papa Francisko,Jumamosi 11 Juni 2022.Wamewasilisha Ripoti ya Kituo cha
Kuchunguza Wanawake Duniani ambapo Papa alisema atakutana na wanachama wote mwezi Mei 2023,kabla ya Mkutano Mkuu huko Assisi.
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Ulikuwa ni Mkutano uliojaa mapendo, zawadi na vichekesho (kama vile vya mweka hazina ambaye aliambiwa na Papa kuwa yeye ndiye aliye na nguvu!), lakini pia hata maelekezo yaliyo wazi kwa
siku zijazo na za sasa za wanawake katika Kanisa na shukrani, kwa kazi iliyofanywa kwa ajili ya wasioonekana kwa mabara matano. Hayo yalisikika wakati Papa Francisko aliwapokea Jumamosi
tarehe 11 Juni 2022, wajumbe wa Baraza kuu la Umoja wa Vyama vya Wanawake Katoliki Duniani (WUCWO/Umofc), ambao mwaka 2021 walianzisha Kituo cha Uchunguzi Duniani kote, ambacho kilitoa
ripoti kuhusu “Athari za UVIKO-19 kwa wanawake katika Bara la Amerika ya Kusini na Caribbean”.
Umoja wa Wanawake Katoliki Ulimwenguni Matokeo ya ripoti hiyo yamekabidhiwa kwa Papa Francisko alipokutana na wawakilishi hao. Tarehe 14 Juni 2022 itawasilishwa hata katika mkutano jijini
Roma na Kardinali Marc Ouellet, rais wa Tume ya Amerika ya Kusini (CAL). Papa Francisko kama alivyosem msemaji wa wajumbe hao waliokutana na Papa ambaye amebainisha kwamba amewahimiza
waendelee na kazi hiyo ambayo sasa imeanza kwa bara la Afrika na akaahidi kwamba mnamo Mei 2023, katika mkesha wa Mkutano Mkuu wao Umfc huko Assisi, atawapokea wanachama wote wa Vyama vya
Wanawake Katoliki Ulimwenguni. Kwa maana hiyo jijini Roma mwezi huo utawaona wanawake wengi kutoka duniani kote, amesisitiza Bi María Lía Zervino, Rais wa Umoja huo, wakati akizungumza na
Vatican News mara baada ya Mkutano huo na Papa Francisko.
Umoja wa Wanawake Katoliki Ulimwenguni Katika mahojiano hayo rais huyo amefafanua mkutano uliovyokuwa na kwamba ulikuwa wa ajabu! Huo ulikuwa ni mkutano wawakilishi wa Wanawake kutoka mabara
yote pamoja na Baba Mtakatifu. Walimshukuru kwa sababu amefanya mengi kwa ajili ya wanawake kwa kipindi cha Upapa, hasa kwa mageuzi yaliyofanywa ya Curia Romana katika hatua za Uinjilishaji
kwenye Katiba ya Kitume' Praedicate Evangelium', ambapo katika Katibua hiyo inaonesha uwazi sasa juu ya wanawake pia ambao wanaweze kuwa wakuu wa Mabaraza ya kipapa. Hotuba ya
kitaalimungu aliyowapatia juu ya kanuni ya huduma na kanuni ya Maria ilikuwa amesema ilikuwa nzuri. Kwani alisema: “ni kweli, kanuni ya Petro, ambayo ni ya kihierarkia, lazima itumike kwa
nafasi ya wanawake, lakini kanuni ya Maria pia ni muhimu zaidi, kwa sababu Kanisa ni mwanamke. Yeye ni mama".
Umoja wa Wanawake Katoliki Ulimwenguni Kwa kujibu iwapo jibu alilotoa Papa Francisko kama limemridhisha kuhusiana na vyama vingi vya wanawake katoliki kuomba kutambuliwa katika huduma, Bi
Lia amejibu kwamba wanafahamu hilo, lakini Umoja wao (WUCWO), kama jumuiya ya umma ya waamini, inao moyo na akili yake katika ushirika na majisterio. Tangu mwanzo wanajua kwamba kungekuwa
vigumu sana kuwa na ufunguzi wa ukuhani wa kike, hivyo wao daima wanajua sababu na kuhusu jinsi ya kushirikiana na Kiti kitakatifu, maaskofu, majimbo na harakati mbali mbali katoliki. Wao
wanafurahia sana kwa kila kitu ambacho Papa Francisko amefanya na wakati huo huo wanajiamini hata kwa ajili ya Ushemasi wa kike(Diakonia), kutokana na kwamba zimeanzisha tume mbili za
kutafakari juu ya sauala hili la ushemasi katika Kanisa. Lakini hili sio lengo lao. kwa sababu wanachotaka ni kuweka manufaa ya wanawake katika huduma ya Kanisa, ambayo si ya wanaume tena,
bali tofauti. Kila kitu kinakuwa tajiri wakati wanaume na wanawake wanafanya maamuzi msingi kwa pamoja.
Umoja wa Wanawake Katoliki Ulimwenguni Kwa upande wa huduma inayotolewa na Umoja wa vyama vya Wanawake Katoliki Ulimwenguni Bi Maria Lia amebainisha juu ya kuwajibika kwa ushirikiano wa
uinjilishaji kwa uso wa kike; na kuwa na uwezo wa huruma, ukaribu, ufahamu, jambo ambalo Kanisa linahitaji leo hii. Papa aliwashukuru sana kwa hilo kwa upendo mkubwa na kwa hakika walihisi
kama kuwa nyumbani na baba yao. Kwa upande wa maelekezo aliyowapatia, Bi Lia alisema, kwanza kabisa, kuchagua mwanamke wa kufanya kazi pamoja na msaidizi wa kikanisa kwa Umoja wao. Baadaye
akawahakikishia kwamba mwaka ujao, kabla ya Mkutano Mkuu uliopangwa kufanyika Assisi mwezi Mei 2023, atakutana ana kwa ana na wanachama wote wa Umoja. Kwa njia hiyo wanawake wote Wakatoliki
wa vyama vyao ulimwenguni wanaalikwa jijini Roma. Mkutano huo pia ulikuwa fursa ya kuwasilisha kwa Papa baadhi ya tafiti zilizofanywa katika miezi ya hivi karibuni, kwa maana hiyo amesema
wametoa matokeo ya kwanza ya ripoti iliyotayarishwa na Kituo cha Kuchunguza Wanawake Duniani, kilichoanzishwa mnamo mwaka 2021, kuhusu athari za UVIKO-19 katika Bara la Amerika ya Kusini na
Carribien ambayo ni kazi ya kutoa sauti kwa wasioonekana.
Umoja wa Wanawake Katoliki Ulimwenguni Je hao ni wakina nani? Ni Wanawake katika nchi zenye vita, bila waume au watoto wakubwa, ambao wanapaswa kutunza familia zao. Wanawake ambao hawawezi
kwenda shule kwa sababu utamaduni wao unahitaji kwamba wanaume pekee ndio wanaweza kusoma. Wanawake wanaoteseka na ukatili wa kijinsia. Mifano ni mingi amesisitiza Bi Lia... Wanawake hawa,
ambao wako hatarini zaidi, hata hivyo ni wale ambao wana nguvu zaidi, ustahimilivu, ambao wanafikiria juu ya hali ya baada ya Uviko. Kwa maana hiyo wao wanakusanya wanayosema na kuyapa
muundo wa kitaaluma ili kuonesha matokeo haya katika ulimwengu, hasa kwa watoa maamuzi.
Akijibu swali namna gani umeunda muundo huo wa kitaaluma? Rais wa WUCWO, amesema kwa kufanya muhtasari wa shuhuda zote na pia ripoti za wataalam kutoka nchi 25 za Amerika Kusini, viongozi
wanaofanya kazi kila siku sehemu mahalia na wanawake walio katika mazingira magumu. Kwa hivyo uzoefu wa moja kwa moja unaopitishwa katika mchanganyiko wa kitaaluma, wenye uwezo wa kuzungumza
kwa lugha rahisi kwa maaskofu, serikali, mashirika ya kiraia, ili kuunda harambee. Bado juu ya athari za Uviko, kufungwa kumesaidia kuongezeka kwa vurugu ndani ya nyumba. Na ni jambo
linalounganisha mabara yote.
Umoja wa Wanawake Katoliki Ulimwenguni Katika suala hili, ni nini kiliibuka katika fundisho hilo? Rais alisema kwa hakika kutengwa hakukuruhusu hata wanawake kuwa na uwezo wa kushirikisha
kile walichoteseka au kupata nafasi ya msaada. Lakini hiyo haikuwa tatizo pekee ... “Hebu fikiria juu ya kazi: wanawake, mara nyingi hawakuwa na kazi ya utaratibu, hawakuwa na pesa za
kufanya hivyo hadi mwisho wa mwezi. Wengi walituambia kuwa “tulikuwa na hofu ya njaa zaidi kuliko Uviko” ! Sawa na elimu, wanawake wengi kutokana na kuanzisha masomo ya mbali, walirudi
nyuma, wao na watoto wao. Na baadaye shida za kimwili kwa sababu katika miezi hiyo Uviko pekee ndiyo ulifikiriwa, wakati wanawake wajawazito, kwa mfano, hawakuweza kupokea matibabu mengine
yanayohitajika. Kisaikolojia ilikuwa uharibifu mbaya, lakini wanawake wenyewe walianza kuunda mitandao na mashirika ili kusonga mbele". Ndiyo maana amezungumzia ustahimilivu, kwamba
kiukweli wana mengi ya kusema katika hawamu baada ya UVIKO.
Na kuhusu ripoti hiyo, waliyomkabidhi Papa Francisko Rais, huyo alisema kwa kuwa alikuwa bado hajasoma na akapokea, hata hivyo aliwashukuru kwa hakika kwamba ni kazi nzito sana ya kisayansi,
iliyofanywa kwa ushirikiano na CELAM. "Pia tulimpelekea hata suala la unyanyasaji, jinsi ya kuzuia katika shule na nyumbani, kwani hapo ndipo shida inapoanzia. Ni kijitabu kilichoandikwa
pamoja na wataalamu, huku utangulizi ukitolewa na Katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, Bi Linda Ghisoni". Wamekichapisha kwa Kiingereza, Kihispania, Kifaransa, na
kukitafsiri katika Kikorea na Kiurdi kwa ajili ya nchi ya Pakistan. Bara la Asia lina furaha sana, kutokana na kwamba tatizo hili lina uzito mkubwa juu ya mabega ya wanawake wa Asia. Kila
mwakilishi wa kanda baadaye alitoa hata zawadi kwa Papa.
Kwa mfano, makamu wa rais wa Uhispania aliwasilisha mwanamke Mzungu, Pilar Bellosillo, rais wa wao (WUCWO), wakati wa Mtaguso wa Pili wa Vatican ambaye Papa Paulo VI alimteua katika kundi la
kwanza la wakaguzi wa hesabu, ambapo mchakato wa kutangazwa kuwa mtakatifu ilianzishwa tayari. Yeye ni mfano kwa wanawake wote, si tu katika bara la Ulaya, lakini pia kwa sababu alikuwa
mlei ambaye alifanya kazi nzuri kwa ajili ya haki na uekumene. Mwakilishi wa Afrika alimpatia Papa Francisko takwimu ya sala zote ambazo wanawake hufanya kwa kujibu ombi lake:
“Niombeeni”. Kwa hivyo Misa, ibada, rozari, kila kitu ... Kutoka bara la Amerika ya Kusini, ilikuwa ya kufurahisha sana: kwa vile Baba Mtakatifu alitania wiki chache zilizopita kwamba
atahitaji tequila kwa ajili ya goti lake, hivyo walimpatia chupa ya tequila.
Mchango wako kwa ajili ya utume mpana zaidi: tuunge mkono ili tupeleke ujumbe wa Papa kwa kila nyumba. 12 Juni 2022, 12:07 Tuma Chapa