Papa:wayahudi na wakristo wanaokiri muumba mmoja wanaweza kufungua njia za amani! - | vatican news

Play all audios:

Katika mkutano na wawakilishi wa Jukwaa la Kimataifa la Kiyahudi,Papa Francisko amebainisha kwamba kila vita siku zote,kila mahali ni kushindwa kwa wanadamu wote.Hakusahau vita nchini
Ukraine kwamba vita vya kufuru ambavyo vinatishia Wayahudi na Wakristo sawa,kwa kuwanyima wapendwa wao,nyumba zao,mali zao na maisha yao yenyewe. NA ANGELLA RWEZAULA – VATICAN. Baba
Mtakatifu Francisko Jumanne tarehe 22 Novemba 2022 amekutana na washiriki (World Jewish Congress), wa Jukwaa la Kimataifa la Kiyahudi ambapo awali ya yote amemshukuru Balozi wake Lauder kwa
maneno yake aliyomwelekea. Ziara yao amesema inashuhudia na kuimarisha uhusiano wa urafiki ambao unawaunganisha Wayahudi na Wakristo tangu Mtaguso wa II wa Vatican, Shirika lao
linajadiliana na Tume kwa ajili ya Mahusiano ya kidini na Uyahudi na ni kwa miaka sasa wanaandaa makongamano makubwa muhimu. Wayahudi na wakatoliki wana ushiriki mkubwa wa thamani ya
tasaufi. Hiyo ni kwa sababu Baba Mtakatifu ameeleza kuwa Tunakiri imani katika Muumba wa Mbingu na dunia ambaye si kwamba alitoa mwanzo wa ubinadamu, lakini alimfinyanga kuwa binadamu kwa
mfano wa sura yake (Mw 1,26). Tunaamini kuwa Mwenyezi hakubaki mbali na uumbaji wake, lakini alijionesha, si kwa kuwasiliano na baadhi tu; Waliotengwa, lakini alielekea sisi wote kama watu.
Kwa njia ya imani na masomo ya maandiko Matakatifu, yaliyoenea katika tamaduni zetu za kidini, tunaweza kuingia katika uhusiano na Yeye na kugeuka kuwa washirika wa utashi wake ulio mwema.
Papa amekutana na washiriki wa Kongamano la Jukwaa la Kimataifa la Wayahudi Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba yake kwa Washiriki hao wa Jukwaa la Kiyahudi amesema tuna hata mtazamo wa
hatima inayofanana ya maisha, inayojikita katika imani ambayo katika mchakato wa maisha, kuwa hatuelekei utupu bali katika kukutana na Aliye juu ambaye anatutunza, kukutana na Yule
ambaye alitoa ahadi kwetu. Katika mwisho wa siku yetu, ufalme wa amani, mahali ambapo kila kitu ambacho kinatishia maisha, kitakuwa na mwisho na kuishi pamoja kibinadamu. Ulimwengu wetu
umegubikwa na vurugu, ukandamizaji na unyonyaji, lakini hayo yote hayana neno la mwisho: ahadi aminifu ya milele inatueleza wakati ujao wa wokovu, wa mbingu mpya na dunia mpya (taz Is
65,17-18; Ap 21,1) mahali ambapo amani na furaha vitakuwa na msimamo wa dhati, mahali ambapo kifo kitafutwa daima, mahali ambapo Yeye atafuta machozi ya kila uso (Is 25,7-8), na mahali
ambapo hakutakuwa na machozi na wala maombolezo ya mahangaiko. (taz Ufu 21,4). Bwana atatimiza wakati huo ujao, na zaidi Yeye mwenyewe atakuwa ndiye wakati wetu ujao. Na ikiwa yapo mawazo
tofauti katika uyahudi na katika ukristo kuhusu jinsi suala hili litakavyokuwa, kuna ahadi ya faraja tuliyo nayo katika jitihada za ulimwengu uweze kukaliwa na historia ambayo tunaishi
iangaze, uwepo wa Yule ambaye alituita kuwa watu wake na kulinda ndugu zetu. Papa amekutana na washiriki wa Kongamano la Jukwaa la Kimataifa la Wayahudi Baba Mtakatifu amesema katika mwanga
wa urithi wa kidini tunaoshiriki, tunaitazama ya sasa kama changamoto inayotuunganisha, kuwa ni himizo la kutenda pamoja. Jumuiya zetu mbili za imani zimepewa jukumu la kufanya kazi ya
kuifanya dunia kuwa ya kindugu zaidi, kupambana dhidi ya ukosefu wa usawa na kukuza haki zaidi, ili amani isibaki kuwa ahadi ya ulimwengu mwingine, lakini ambayo tayari ni ukweli katika
ulimwengu huu. Ndiyo, njia ya kuishi pamoja kwa amani ambayo huanza na haki na ambayo, pamoja na ukweli, upendo na uhuru, ni moja ya masharti msingi ya amani ya kudumu duniani (taz. Waraka
wa Kitume wa Papa Yohane XXIII wa Pacem in terris, 18.20.25). Ni wanadamu wangapi, walioumbwa kwa sura na mfano wa Mungu, wameharibiwa utu wao, kutokana na ukosefu wa haki unaoisambaratisha
sayari na kuwakilisha sababu ya msingi ya migogoro mingi, bonde kavu ambamo vita na vurugu vinaendeshwa! Yeye ambaye ameumba kila kitu kwa utaratibu na maelewano anatualika kuondoa bonde la
dhuluma ambalo linazamisha kuishi pamoja kidugu duniani, kama vile uharibifu wa mazingira unavyohatarisha afya ya dunia. Papa amekutana na washiriki wa Kongamano la Jukwaa la Kimataifa la
Wayahudi Mambo yaliyoanzishwa ya pamoja na dhati kuelekea kuhamasisha haki yanahitaji ujasiri, ushirikiano na ubunifu. Kwa familia kubwa ya imani, uwezo wa kuwa na imani kwa Mwenyezi na
kuanza kutazama Yeye badala ya mambo ya upendeleo wa kidunia, ambayo daima ni ya muda na sio ya kudumu, kwa namna ya pekee yasiyo na uwezo wa kukumbatia upamoja. Kinyume chake imani thabiti
katika wazo kwamba, kila mtu ni sura na mfano wa aliye juu, inatualika kutembea pamoja kuelekea ufalme. Maandiko matakatifu baadaye yanatukumbusha kwamba kidogo au kikubwa hatuwezi
kukifanya ikiwa Mungu hatupatii nguvu na utashi.” Mungu hasipojenga nyumba waijengao wanafanya kazi bure (Sal 127,1). Katika maneno mengine, shughuli zetu za kisiasa, kiutamaduni na kijamii
kwa ajili ya kuboresha ulimwengu ile ambaye tunaita “Tiqqun Olam”, haiwezi kuleta ufanisi ikiwa haina sala, bila ufunguzi wa kidugu kwa viumbe wengine katika jina la Muumba mmoja ambaye
anapenda maisha na kubariki wahudumu wa amani. Leo hii katika kanda nyingi za ulimwengu amani inatishiwa, Baba Mtakatifu amesema tujitambue pamoja kuwa vita , kila vita daima na kila
mahalii ni kushindwa kwa ubinadamu! Papa Francisko amekumbuka kwa maana hiyo nchini Ukraine, vita vya kashfa ambayo vinatisha Wayahudi na Wakristo, na wakati huo huo kwa njia nyingine
kuwanyima wao upendo, nyumba zao, mali zao na maisha yao wenyewe! Ni utashi wa kina tu wa kukaribiana mmoja na mwingine na katika kujadiliana kindugu inawezakana kutengeneza ardhi ya amani.
Kama wayahudi na Wakristo tutafute kufanya kila kiwezekanacho cha ubinadamu unaowezekana kusitisha vita na kufungua njia za amani. Papa amehitimisha akiwashukuru kwa moyo ujio wao. Na
Mwenyezi ambaye ana mpango wa amani na wala sio wa mabaya (Yer 29,10 abariki matendo yao mema. Na awasindikiza katika mchakato wa safari na kuwaongoza pamoja juu ya njia ya amani. Papa
akutana na washiriki wa Kongamano la Jukwaa kimataifa la Kiyahudi