Kilio cha papa dhidi ya ukoloni mpya - | vatican news

Kilio cha papa dhidi ya ukoloni mpya - | vatican news

Play all audios:


Mkumbatio wa Papa Fransisko kwa watu waliojaribiwa na migogoro na umaskini,ambapo kutoka kwa Mrithi wa Petro hunapokea msukumo wa kujikomboa dhidi ya aina zote za unyonyaji. NA ANGELLA


RWEZAULA, - VATICAN Nchi kubwa na iliyojaa maisha, pafu la pili la sayari baada ya Amazon shukrani kwa upanuzi wa msitu wake wa kitropiki, ambao umeporwa kwa pupa. Nchi yenye maliasili


nyingi, iliyokumbwa na vurugu kama ngumi ya tumbo, ambayo inaonekana kukosa pumzi kwa muda. Haya ni kati ya maneno  mazito katika hotuba yake, mara baada ya kulakiwa na maelfu ya watu wa


rika zote waliofurika barabarani kutoka uwanja wa ndege wa Ndolo hadi katikati mwa jiji kuu la Kinshasa, ambapo Baba Mtakatifu alizindua ujumbe wake wa kwanza katika Jamhuri ya Kidemokrasia


ya Congo na kwa Afrika yote. Katika bustani ya Ikulu ya Taifa, akiwa ameketi karibu na Rais Felix Tshisekedi Tshilombo, Mrithi wa Petro alizungumza maneno ya kuunga mkono Wakongo wote ambao


wanapinga majaribio ya kugawanya nchi iliyovuka kikomo kwa ghasia na kwa mara nyingine tena akakumbuka kitu cha unyonyaji huko Congo na  zaidi kwa ujumla kwa bara zima la Afrika. “Baada ya


ule wa kisiasa, ukoloni wa kiuchumi umeibuka ambao ni utumwa zaidi”, alisema Papa Francisko. Hotuba ya Papa huko DRC Ni ukoloni wa hila zaidi na usio na kelele zaidi, unaowaondoa watu wa


Kiafrika uhuru na kujitawala. Kwa hiyo, Papa aliongeza, kusema  kwamba huko Congo “umefikia kama kitendawili cha matunda ya ardhi yake kufanywa nchi kuwa ya kigeni kwa wakazi wake. Kwa


sababu sumu ya pupa imefanya damu yake kuwa almasi. Ni janga ambalo mbele yake ulimwengu ulioendelea zaidi kiuchumi mara nyingi hufunga macho, masikio na midomo yao”. Viongozi wakisikiliza


hotuba ya kwanza ya Papa Papa Fransisko kwa hiyo alitaka kufika hapo ili kuwakumbatia watu hao waliojaribiwa na migogoro na umaskini ili kuhakikisha kwamba macho, masikio na midomo ya wote


inafunguka na kukumbusha juu ya migogoro iliyosahaulika ambayo inaunda vipande vingi vya Vita vya tatu vya Kidunia na matokeo yake ya mfumo wa kiuchumi na kifedha ambao unaua kwa sababu


hauweki  mtu katikati, bali ni mungu pesa. “Nchi hii na bara hili, alisema Papa katika hotuba yake ya kwanza huko Kinshasa kwamba wanastahili kuheshimiwa na kusikilizwa, wanastahili nafasi


na tahadhari: toeni mikono yenu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, iondoeni katika bara la  Afrika! Acha kuisumbua Afrika: sio mgodi wa kunyonywa au udongo wa kuporwa",


alisisitiza. Tahariri ya Tornielli kuhusu hotuba ya Papa 31 Januari 2023