Kard. Becciu:padre sturzo ni shuhuda wa injili ya haki na tumaini! - | vatican news

Kard. Becciu:padre sturzo ni shuhuda wa injili ya haki na tumaini! - | vatican news

Play all audios:


Katika kufunga mwaka uliotolewa kwa Padre Sturzo,Kardinali Becciu katika mahubiri wakati wa Misa Takatifu iliyoadhimishwa huko Caltagirone,wilayani Catania nchini Italia amekumba sura ya


Padre wa Sicilia ambaye hata leo hii anatia moyo wa kukuza zile thamani za kibinadamu na Wakristo ambao huunda urithi bora na muhimu barani Ulaya. NA SR. ANGELA RWEZAULA – VATICAN Sura ya  


kuhani na  aliyekuwa kiongozi  wa serikali, kwa jitihada zake alifanya  kuibuka kwa jumuiya na jamii halisi ya kidemokrasia. Na huyo ni Padre Luigi Sturzo, ambaye amebainishwa na Kardinali


Giovanni Angelo Becciu, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la kuwatangaza Watakatifu wakati wa hitimisho la Mwaka uliokwa  “kumbukumbu ya Padre Sturzo” aliyetangazwa kwa mwaka wa Chama cha Watu


wa Italia. UTAKATIFU NI KUFANANA NA MUNGU Katika misa hiyo Jumamosi jioni majiara ya Ulaya tarehe 18 Januari 2020, Kardinali Becciu amesema, kuishi upendo wa Mungu na jirani ndiyo njia ya


kufika  utakatifu na ambao unajikita katika kufuata Injili. Sura hii ya kihistoria ya ukatoliki nchini Italia, imejionesha katika jitihada za kijamii kwa wakatoliki na ambao bado wanapaswa


kupyasha katika  ushiriki wa maisha hai ya ukatoliki katika nchi. Na hizi ndizo zilikuwa jitihada za mpango wa maisha ya watu kijamii, na mhuri wa kidemokrasia wa kikristo.  Alikuwa shuhuda


katika Jamii hasa katika Injili ya haki na matumaini. Mtumishi wa Mungu Padre Sturzo alijikita na roho ya uadilifu, huru na nguvu katika uwanja wa kisiasa: Aliweka  yote katika kitovu cha


Mungu na sababu ya maisha yake, kabla ya kila kitu! Katika sala alikuwa anachota nguvu ya kiroho na kutoa huduma kwa wema wa pamoja huku akipinga pia hata uzoefu mgumu wa kutokuelewana, kwa


madai na hata kukataa uchungu amesema Kardinali Becciu. KUKUZA URAIA  WA NCHI Padre Sturzo, Kardinali Becciu amemeendelea kusema,  Yeye hakuacha kuelekeza na kuheshimu mipaka sahihi kati ya


siasa na dini, katika imani hiyo, Serikali  na Kanisa zinaalikwa  kushirikiana kwa ajili ya ustawi wa watu wale wale, lakini kwa utofauti ulio wazi wa nafasi za majukumu na ustadi,


amebainisha Kardinali Becciu. Aidha akiendelea, kwa mujibu wa Kardinali Becciu, Padre Sturzo alikuwa mwamasishaji mzuri  na mlezi wa maono ya kikristo  katika  uraia wa serikali ambao siyo


upinzani au tofauti, lakini ni heshima na ushirikiano kati ya jumuiya ya raia na ule ya kikanisa kwa ajili ya wema wa kweli wa mwanadamu na familia ya binadamu. USHIRIKI WA MAISHA YA


KIJUMUIYA NA TAA Hata leo hii Padre Sturzo anakumbusha wakristo kwamba wanapaswa kuwajibika katika kushiriki katika  maisha ya kijumuiya, huku wakijitahidi hata katika masuala ya kisiasa


ambayo  ni mtindo ulio wa juu kabisa wa upendo kama alivyokuwa amethibitisha hata Mtakatifu Paulo VI. Ni wito uliowekwa wa huduma na ambao unapatikana kwa maana ya  hisia za taasisi. Vile


vile hata leo hii, anaongeza Kardinali Becciu kuwa, Padre Sturzo anaendelea kuangaza safari ya Italia na Kanisa.Ushuhuda wake wa imani na mafundisho yake  Jamii-siasa, ni urithi mkubwa kwa


nchi ya Italia na ambao unazidi kuombwa ueleweke, uhifadhiwe,utafakariwe, na kushuhudiwa hata nje ya mipaka ya kitaifa. Padre Sturzo alikuwa ni mtu wa huduma ya pamoja ambayo hata leo hii


yeye anzaidi kualika na kutia moyo wa kukuza zile thamani za kibinadamu na wakristo ambao wanaunda utajiri bora na muhimu kwa urithi wa Ulaya. Yeye alitoa maisha yake kwa ustaarabu ambao


katika karne nyingi umesababisha kuibuka kwa jamii za kidemokrasia za kweli. Bila misingi ya maadili, Kardinali amehitimisha  demokrasia  iko hatari ya kudhoofika kwa muda na hata kutoweka!