Askofu josé lampra cà wa jimbo katoliki la bissau, guinea bissau - | vatican news

Play all audios:

Askofu José Lampra Cà wa Jimbo Katoliki la Bissau, Guinea-Bissau alizaliwa tarehe 5 Januari 1964 huko Blom nchini Guinea-Bissau. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 27
Desemba 1997 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Mwaka 2011 akawekwa wakfu kuwa Askofu na Mwaka 2020 akateuliwa kuwa Msimamizi wa Kitume wa Jimbo la Bissau, Guinea-Bissau. NA PADRE RICHARD A.
MJIGWA, C.PP.S. – VATICAN. Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Msaidizi José Lampra Cà wa Jimbo Katoliki la Bissau, Guinea-Bissau kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Bissau,
Guinea-Bissau. Kabla ya uteuzi huu, alikuwa ni Askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bissau, Guinea-Bissau. Itakumbukwa kwamba, Askofu José Lampra Cà wa Jimbo Katoliki la Bissau,
Guinea-Bissau alizaliwa tarehe 5 Januari 1964 huko Blom nchini Guinea-Bissau. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 27 Desemba 1997 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili
ya Jimbo Katoliki la Bissau, Guinea-Bissau. TAREHE 13 MEI 2011 BABA MTAKATIFU MSTAAFU BENEDIKTO XVI AKAMTEUWA KUWA ASKOFU MSAIDIZI WA JIMBO KATOLIKI LA BISSAU, GUINEA-BISSAU na kuwekwa
wakfu kuwa Askofu tarehe 12 Novemba 2011 na Askofu José Câmnate na Bissign wa Jimbo Katoliki la Bissau, Guinea-Bissau. Tarehe 11 Julai 2020 Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Msimamizi
wa Kitume “Sede Vacante ad nutum Sanctae Sedis” Jimbo Katoliki la Bissau, Guinea-Bissau. Yaani kama Msimamizi wa Kitume, alikuwa anawajibika moja kwa moja na Vatican katika masuala yote ya
uongozi wa JimboKatoliki la Bissau, Guinea-Bissau. Na tarehe 10 Desemba 2021, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Bissau, Guinea-Bissau.