Dk.Ruffini:Dira ya Sinodi ni Kanisa la kukaribisha wote

Dk.Ruffini:Dira ya Sinodi ni Kanisa la kukaribisha wote

Play all audios:


Dk. Paolo Ruffini,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano na Rais wa Tume ya Habari ya Sinodi 4 hadi 29 Oktoba 2023.  Vatican Dk.Ruffini:Dira ya Sinodi ni Kanisa la kukaribisha wote Ni


kawaida kwetu kujiuliza:tuko wapi ulimwenguni,tuko wapi kwenye safari yetu?Tumefikia wapi? Na wapi?Na zaidi ya yote,je,mkutano huu wa maaskofu kutoka mabara yote hapa Roma,pamoja na sehemu


ndogo ya watu rahisi waliobatizwa ulisaidia?Ni maswali ya Dk.Ruffini,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano na Rais wa Tume ya Habari ya Sinodi. Na Angella Rwezaula, - Vatican.


Kukutana pamoja, kusali pamoja, kusikiliza neno la Mungu pamoja na kusikiliza kila mmoja kumesaidia kugundua tena kile kinachotuunganisha kuwa katika Kristo, kwa kutembea pamoja, ardhi nzuri


ambapo mbegu inaweza kukua; kushuhudia kwamba njia nyingine ya kuwa pamoja inawezekana; kuthamini daima, watu wa Mungu waliounganishwa kwa ubatizo, kile kinachotuunganisha na kamwe kile


kinachotutenganisha... Ndiyo maneno ambayo Dk. Paulo Ruffini, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano na aliyekuwa Rais wa Tume ya Habari ya Sinodi ambaye kila siku ya siku za Sinodi


akiwa amezungukwa na wasemaji aliweza kutoa habari ya kile ambacho kilikuwa kinaendelea tangu kuanza kwa Sinodi ya XVI ya Maaskofu kuanzia tarehe 4 -29 Oktoba 2023, ikiongozwa na Mada


kuu:Kwa Ajili ya Kanisa la Kisinodi: Ushirika, Ushiriki na Utume. Hata hivyo Sinodi hii imegawanyika katika awamu mbili ambapo ya kwanza imehitimishwa na ya pili ni Oktoba 2024.


Mama baba wa Sinodi na Mama   (Vatican Media) Kwa njia hiyo mara baada ya hitimisho la Sinodi hiyo, akitoa maoni yake katika Makala ya  Habari za Kikanisa SIR la Baraza la Maaskofu Italia


kuhusiana na tukio hilo muhimu, Dk Ruffini anabainisha kuwa  "baada ya kufikia hatua ya nusu ya Sinodi hii, ambayo inatutaka tujifikirie upya kama Kanisa, tunajikuta tukistaajabishwa katika


ulimwengu wenye mgawanyiko ambao "umepoteza njia ya amani, ambayo umempendelea Kaini kuliko Abeli" (Tazama Sala ya Papa Francisko ya amani ya 27.10.2023); sayari ambayo "inabomoka na labda


inakaribia mahali pa kuvunjika" (Papa Francisko, Laudate Deum,2). Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano kwa hiyo anasisitiza kuwa "Ni kawaida kwetu kujiuliza: tuko wapi ulimwenguni, tuko


wapi kwenye safari yetu? Tumefikia wapi? Na wapi? Na zaidi ya yote, je, mkutano huu wa maaskofu kutoka mabara yote hapa Roma ulisaidia, pamoja na sehemu ndogo ya "watu rahisi waliobatizwa"?


Je  ulisaidia nini?


Washiriki wa Sinodi Akiendelea Dk Riffini anabainisha kuwa, “Hati ya muhtasari inaishia kwa kunukuu Injili ya Marko (Mk 4.30 ) isemayo "Ufalme wa Mungu umefanana na mbegu ya haradali ambayo


ikipandwa ardhini ni ndogo kuliko mbegu zote, lakini inakuwa kubwa sana hivi kwamba ndege wa angani wanaweza kujificha kwenye kivuli chake. " Na hivyo  ndivyo ilivyokuwa kwa ajili ya


kukusanyika, kusali pamoja, kusikiliza neno la Mungu pamoja na kusikilizana kwa ajili ya kugundua tena kile kinachotuunganisha kuwa katika Kristo; kutembea pamoja, ardhi nzuri ambapo mbegu


inaweza kukua." Dk. Ruffini aidha anabainisha kwamba katika Sinodi hii ni wazi ilikuwa ni ushuhudia kwamba njia nyingine ya kuwa pamoja inawezekana. Na hii ni kwa sababu lazima kuthamini


kila wakati, watu wa Mungu waliounganishwa kwa ubatizo, kile kinachotuunganisha na kamwe kile kinachotutenganisha. Kuelewa kwamba jukumu la ushirikiano ambalo kila mtu anaitwa, hata  katika


utofauti wa karama na huduma ni huduma na sio nguvu. Vile vile ni kugundua upya  kwa jinsi gani hotuba ya Yesu juu ya umaskini inatuhusu sisi sote, kama watu na kama taasisi. Zaidi pia ni


kupendekeza na kuepuka ukasisi wowote (ule wa walei na ule wa mapadre waliowekwa wakfu).


Kujadili na kutembea pamoja   (Vatican Media) Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano aidha alisisitiza kuwa ni kugundua tena umuhimu wa kila moja; na zaidi ya ushirika wote unaotufanya kuwa


wamoja, washiriki wa mtu mwingine. Kutafakari juu ya nafasi ya wanawake, ambao walikuwa wa kwanza kutangaza ufufuko wa Yesu. Kutoa msukumo mpya kwa uekumene. Kuwa Kanisa la kukaribisha watu


wote. Na zaidi kila mtu, ambapo hakuna mtu aliyetengwa. Kuwa Kanisa ambalo halifikirii kulingana na migawanyiko na alama za ulimwengu, lakini linalojiuliza kila wakati ikiwa Yesu angefanya


nini akikabiliwa na kaka au dada aliyejeruhiwa. Na ni kwa jinsi gani angehakikisha kutowatenga na ukombozi. Rais wa Tume ya Habari ya Sinodi aidha alithibitisha jinsi ambavyo kuna changamoto


nyingi ambazo tunakabiliana nazo kama Kanisa. Zinahusu ukuhani, ushemasi, huduma zisizowekwa wakfu, maisha ya wakfu, familia na hali ngumu za ndoa; Huduma ya Kipetro, Uekumene, mawasiliano


katika enzi ya kidijitali. Pia zinahusu mada yenye utata wa utambulisho wa kijinsia na mwelekeo wa kijinsia.


Kila siku Dr Ruffini na tume yake walihabarisha juu ya kinachoendelea cha Sinodi   (Vatican Media) Dk. Ruffini alisisitiza kuwa, "lakini yote hayo ni upendo unaojumuisha wote. Sheria moja tu


inaelezea Kanisa la Sinodi inayokubalika:ya  upendo; ubunifu wa kimisionari wenye msingi mzuri, vumilivu, wema; “si lenye wivu, si lenye majivuno, si lenye kuvimba” (rej.1Kor 13:4). Hivi


ndivyo Mkutano ulituambia ambao umehitimishwa hivi karibuni. Na imetuonesha dira na siyo orodha ya mambo. Mamilioni, mabilioni ya watu ni kama msafiri aliyesafiri katika barabara kati ya


Yerusalemu na Yeriko. Kwa hiyo hatuwezi kusema sikujua. Kwa hili tutahukumiwa (rej. Mt 25).” Anahitimisha maoni yake Dk. Paolo Ruffini, Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano na aliyekuwa


Rais wa Tume ya Habari ya Sinodi iliyaonza tarehe 4 hadi 29 Otoba 2023.


Wakati wa kutoa taarifa ya sinodi   (Vatican Media) DK.Ruffini baada ya Sinodi Mchango wako kwa ajili ya utume mpana zaidi: tuunge mkono ili tupeleke ujumbe wa Papa kwa kila nyumba. 04


Novemba 2023, 12:58 Tuma Chapa