Congo: ebola bado ni changamoto katika kanda husika! - | vatican news

Play all audios:

Pamoja na migogoro inayo endelea katika kanda ya Congo (DRC) na kuwakilisha matatizo makubwa ya kuweza kuingilia kati, jibu la haraka la utoaji wa huduma katika maadhi ya vituo mbalimbali
vya afya kwa Madaktari wasio kuwa na Mipaka, wanaendelea kugawa vifaa na huduma muhimu katika dharura hiyo SR. ANGELA RWEZAULA - VATICAN Ni zaidi ya miezi miwili tangu kuanza kwa ugonjwa wa
Ebola huko Kaskazini ya Kivu( DRC). Mwaka huu hali bado siyo nzuri na haijathibitiwa, ambapo kesi mpya zaidi zimejitokeza katika kilimeta 100 kuelekea kanda ya kati ya nchi. Mara baada ya
uthibitisho wa ugonjwa huo tarehe Mosi Agosti, Madaktari wasio na Mipaka, walianza mara moja shuguhuli yao kwa ushirikianoa na mantiki ya mpango wa Ofisi ya Waziri wa Afya nchini DRC.
Pamoja na migogoro inayoendelea katika kanda hiyo na kuwakilisha matatizo makubwa ya kuingilia kati, lakini jibu la haraka katika maadhi ya vituo mbalimbali vya afya wanaendelea kugawa vifaa
na huduma muhimu katika dharura hiyo. KADHALIKA KUNA BADHI YA TIBA MPYA AMBAYO INAWEZA KUCHUKUA NAFASI MUHIMU kutoa jibu la haraka na mwafaka wa virus vya Ebola. Vipimo vya damu vinavyo
chukuliwa katika maabara kwenye vituo vya kutibu, vinasaidia madaktari kuanza kwa haraka na kutoa matibabu kwa wagonjwa. Kwanza wanatumia madawa ya aina tano katika mwendelezo wa matibabu ya
mgonjwa na uwezekano wa kufanyia majaribio ya maana katika tiba hizi mpya kati ya wagonjwa wa Ebola kwa masaa 24, baada ya kuthibitisha uchanya wa virus. Vifo kati ya wagojwa wa Ebola ni
kubwa ambayo ni sawa na asilimia karibu 50%. Madawa mapya yana nguvu ya kuongeza uwezekano wa kuishi, kwa mujibu wa utafiti wa madaktari. Kadhalika maafisa wa afya nchini Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC) wamethibitisha watu 24 zaidi wamefariki dunia kutokana na virusi vya ugonjwa wa Ebola mashariki mwa nchi hiyo katika kipindi cha wiki iliyopita. Maafisa hao wa
Afya wametoa wito kwa wakazi wa eneo hilo kuchukua hatua za kujikinga dhidi ugonjwa huo hatari. Makundi ya waasi yamekuwa yakiendeleza uhalifu mpakani mwa Rwanda na Uganda hali ambayo
imefanya kuwa ngumu jitihada za kutoa huduma za kimatibabu. Hadi sasa kesi 216 zimegunduliwa na kati ya hizo kesi 181zimethibitiwa watu 104 wamekufa na 57 wamepona. MAENEO MENGINE YENYE
VIRUS VYA EBOLA PIA NI KARIBU NA MPAKA WA UGANDA HATA HIVYO KWA MUJIBU WA WATAALAM HAO WANASEMA HALI YA EBOLA siyo kwamba inazidi kuongezeka sana, lakini hali inabaki ya kutia wasiwasi.
Wapo wangonjwa waliothibitiwa wa BENI NA BUTEMBO, LAKINI PIA HATA MAENEO MENGINE YA NDANI ZAIDI YANAYOPAKANA NA UGANDA. Hayo yamethibitiwa na Laurence Sailly mratibu wa dharura wa Madaktari
wasio kuwa na mipaka. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini New York, Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric ameonya kuwa ghasia za hivi karibuni
nchini humo zinakwamisha juhudi za kuudhibiti ugonjwa huo. MMOJA MIONGONI MWA WAATHIRIKA ni fundi bomba ambaye anafanyakazi na kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa katika ukanda
huo, amepata maambukizo ya virusi vya Ebola alipokuwa akienda kwa mganga wa kienyeji ambaye anadaiwa kumhudumia mmoja wa waathirika wa ugonjwa huo. Mapema mwezi huu Baraza la Usalama la
Umoja wa Mataifa linafanya ziara ya dharura kuelekea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kufuatia mapigano makali nchini humo ambayo yametatiza jitihada za kudhibiti kuzuka kwa virusi vya
Ebola. Mapigano makali kati ya makundi yaliyojihami katika mji wa Beni Mashariki mwa nchi yamewalenga pia wahudumu wa afya wa Umoja wa Mataifa na kupunguza kasi ya vita kuzuia kuenea kwa
Ebola nchini DRC