Chanjo ya mpox kuchukuwa muda mrefu zaidi kongo

Play all audios:

Mkuu wa timu ya kukabiliana na mpox nchini humo, Cris Kacita, ameonya kuwa kampeni ya kusambaza chanjo inaweza kuchukuwa muda mrefu kuliko siku kumi zilizotarajiwa mwanzoni. Kampeni ya
chanjo ya mpox nchini Kongo ilizinduliwa mwezi huu katika eneo la mashariki lililoathirika zaidi. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, wakaazi wa jimbo la Kivu Kaskazini kulikoanza
kutolewa chanjo hiyo, wanaonekana kutofahamu mengi na wana mashaka nayo. Kampeni hiyo ya chanjo ni hatua muhimu katika juhudi za kudhibiti mripuko wa ugonjwa huo katika kitovu chake, na
ambao sasa umeenea katika mataifa mengine mengi ya Afrika.