Papa francisko:wanawake ni mashuhuda wa kwanza wa ufufuko! - | vatican news

Papa francisko:wanawake ni mashuhuda wa kwanza wa ufufuko! - | vatican news

Play all audios:


Papa Francisko anasema"Tutoke katika hofu zetu,tutoke katika uchungu wetu.Siku zote unampata Bwana katika safari ya kumtangaza.Mtangaze Bwana nawe utakutana naye.Mtafuteni Bwana nanyi


mtakutana naye.Siku zote katika hoja,lakini kutangaza ni jambo moja tofauti na propaganda na kugeuza imani ni jambo jingine. NA ANGELLA RWEZAULA, - VATICAN Leo hii Injili inatufanya tuishi


uzoefu wa  mkutano wa wanawake na Yesu Mfufuka katika asubuhi ya Pasaka. Inatukumbusha jinsi alivyokuwa na  wanawake wafuasi, walio kuwa wa kwanza kumwona na kukutana naye. Ndivyo Baba


Mtakatifu Francisko ameanza Tafakari yake, katika Siku ya Jumatatu ya Pasaka, tarehe 10 Aprili 2023 ambayo kiutamaduni uitwa Jumatatu ya Malaika. Kwa maana hiyo Papa amesema tunaweza


kujiuliza ni kwa nini kuwa na wao?  Ni kwa sababu mbili rahisi, kwa sababu walikuwa wa kwanza kwenda kaburini. Kama wafuasi wote, hata wao walikuwa wanateseka kuona jinsi ambavyo suala hili


la Yesu lilihitimishwa; lakini kinyume na wengine, hawakubaki nyumbani wamegandama na huzuni na  hofu na hivyo asubuhi na mapema wakati jua linachomoza, walikwenda kuabudu mwili wa Yesu


wakichukua mafuta yanayonukia. Kaburi lilikuwa limefungwa na wao walikuwa waweze kuomba ili kutolewa jiwe lile (Mk 16,1-3). Lakini utashi wao wa kutimiza ishara ya upendo huo ilikuwa ni kila


kitu! Hawakukata tamaa, waliondoka na hofu zao na uchungu wao. Na tazama ndio njia ya kumpata Bwana. Waamini katika Sala ya Malkia wa Mbingu 10 Aprili 2023   (Vatican Media) Katika Injili


ilivyoandikwa,ni kwamba wanawake walipofika waliona kaburi tupu, kwa hofu na furaha nyingi walikimba kuwapasha wanafunzi wake habari (Mt 28,8). Na wakati huo wanakwenda kutoa taangazo hilo,


tazama Yesu alikuja kukutana nao.  Papa ameongeza kusema kwamba hapo “Tuwe makini na hili kwani Yesu alikutana nao wakati wanakwenda kumtangaza. Ni nzuri hiyo: wakati tunapomtangaza Bwana,


Bwana anakuja kwetu. Wakati mwingine  tunafikiria ni jinsi gani ya kukaa karibu na Mungu kwa kubaki naye karibu sana, kwa sababu tunapojiweka tayari kuanza kuzungumza baadaye  ndipo zinafika


hukumu, masengenyo,na wakati mwingine hatujuhi namna ya kujibu maswali fulani au uchochezi na kwa hiyo ni vema kutozungumza. Kinyume chake, Bwana anakuja wakati tunaanza kumtangaza. Hivyo


basi hayo wanatufundisha wanawake, kwamba Yesu anakuja kukutana wakati tunamshuhudia”, Papa alisisitiza. Uwanaja wa Mtakatifu Petro   (Vatican Media) Baba Mtakatifu Francisko kwa maana hiyo


ametaka kuonesha mfano kwamba inawezekana ilitokea mara nyingi kupokea habari za kushangaza, kwa mfano kuzaliwa kwa mtoto. Kwa hiyo moja ya mambo ya kwanza tufanyayo ni kushirikisha habari


njema hiyo kwa marafiki. Na kwa kusimulia, huku tukirudia hata sisi wenyewe,na kwa namna moja tunafanya tena kuishi hisia hizo zaidi kwetu sisi. Ikiwa hili linatokea kwa habari njema, hivyo


ilitokea bila kuisha zaidi kwa ajili ya Yesu ambaye sio habari njema tu na wala taarifa nzuri zaidi ya maisha,  lakini ni maisha yenyewe, Ufufuko na uzima (Yh 11, 25). Kila tunapomtangaza,


bila kufanya propaganda, au msimamo mkali, lakini kwa heshima na upendo kama zawadi nzuri zaidi ya kushirikisha, hivyo ndivyo Yesu anakaa tena zaidi ndani mwetu. Waamini katika Uwana wa


Mtakatifu Petro   (VATICAN MEDIA Divisione Foto) Baba Mtakatifu Franciso ameendelea kusema  kuwa tufikirie tena wanawake wa Injili, kwamba kulikuwa na Jiwe lililofunga lakini pamoja na hayo


wao walikwenda kaburini; kulikuwa na mji wote ambao ulikuwa umemwona Yesu msalabani na licha ya hayo walikwenda katika mji kumtangaza aliye hai. Inapotokea kukutana na Yesu, hakuna kizingiti


ambacho kinaweza kuzuia kumtangaza! Ikiwa kinyume chake tunazuia sisi furaha yake, labda ni kwa sababu bado hatujamtambua kiukweli. Baba Mtakatifu amesisitiza kwamba mbele ya uzoefu wa


wanawake, tujiulize: ni mara ngapi ya mwisho tulimshuhudia Yesu? Leo hii je ninaweza kufanya nini ili watu ambao ninakutana nao wapokee furaha ya tangazo? Na bado, mwingine akifikiria kuwa


“mtu huyo ni mtulivu, ana furaha, ni mwema kwa sababu amekutana na Yesu? Tuombe Mama ambaye atusaidie kuwa na furaha ya kuwa watangazaji wa Injili”, amehitimisha Papa. Tafakari ya Papa J3 ya


Pasaka 10 Aprili Jumatatu ya Pasaka