Kard.Tagle,Injili ya Uumbaji:Utume ni zawadi kwa Kanisa lote

Kard.Tagle,Injili ya Uumbaji:Utume ni zawadi kwa Kanisa lote

Play all audios:


Kardinali Luis Antonio Tagle, Kardinali Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu, wakati anazungumza kweny radio Vatican juu ya utume wa kimisionari uliokabidhiwa kwa wahudumu wa Laudato si'


wa Harakati Katoliki Ulimwenguni kwa ajili ya Tabianchi na wahudumu wengine wa kichungaji, vijana, watu wenye mapenzi mema amesema: “Katika utume wa Kanisa kila mbatizwa amepokea Roho


Mtakatifu zawadi ambayo inapaswa kuendelezwa kwa kushiriki katika utume wenyewe na kuhusu suala la Laudato si’,  ni utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja”.


Alithibitisha hayo mara tu baada ya Papa Franciko Jumapili wakati wa Sala ya Malkia wa Mbingu alikuwa amezungmzia juu ya utume wa kueneza Injili ya Kazi ya Uumbaji na kuanza utunzaji wa


mazingira nyumba yetu ya pamoja. Katika mtazamo wa kumbukumbu ya miaka sita ya Waraka wa Papa Francisko juu ya utunzaji wa nyumba ya pamoja, uliochapishwa mnamo tarehe 24 Mei 2015, na katika


Wiki ya Laudato Si, ambayo imehitimisha mwaka maalum uliotangazwa na Papa kutafakari na kujikita kwenye matendo ya dhati ya  waraka huo, vile vile  Kardinali Tagle ameongoza mkutano wa


maombi katika Shirika la Watawa Wafranciskani (OFM) Roma.


Katika siku ya Pentekoste, siku ya kushuka kwa Roho Mtakatifu ambaye alitoa mwanzo wa utume wa Kanisa au kuzaliwa kwa Kanisa, Kardinali Tagle amesema Pentekoste ni kuonesha kuwa Kristo


aliyefufuka anandelea kubaki nasi.  Wito wa Kardinali ni kuwa shuhuda wa ukweli wa ulimwengu, hata baada ya wakati huu ambao ni wa mgogoro uliokumbwa na janga la virusi vya covid-19. Kufanya


uzoefu wa Kristo ni kuelewa kuwa Yesu anatusindikiza kama alivyofanya kwa wafuasi wake. Utume kama wito kwa ajili ya maisha yote ni hata kusindikiza wengine na kubaki kufanya hatua moja


moja na si kurudi nyumba


Kwa upande mwingine, ameunga mkono wa maneno ya Padre Augusto Zampini, katibu msaidizi wa Kitengo cha Baraza la Maendeleo Fungamani ya Binadamu na mjumbe wa mwelekeo wa Tume ya Vaticani


Covid-19. Padre Zampini yeye alisema Injili ya Uumbaji imeunganishwa na Kanisa linalotoka nje, kwa maana ni Kanisa ambalo hutunza nyumba yetu ya pamoja na ya wengine kila mahali kwenye


sayari hii. Huu ndio uzuri wa maana ya kimisionari wa kuleta ujumbe wa Injili na Laudato si ', wa utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja na wengine, katika kila sehemu ya sayari, katika kila


sekta ya jamii, pia kukumbuka jinsi Papa ambavyo anaomba mabadiliko makubwa ya uchumi iliougua, kwa sababu husababisha ukosefu wa usawa, magonjwa ya kijamii, mizozo na uharibifu wa kazi ya


uumbaji, ameongeza Padre Zampini.


Kutoka Rio de Janerio, Nairobi, Washington, Roma, Assisi limefika jibu la ndio la utume wa kimisionari, kuchukua jukumu la Wahuishaji ili kusikiliza kilio cha Dunia na maskini, wale


waathiriwa wa shida na mateso katika nchi ya India kama, ilivyo Brazil ambapo Padre Michael Perry, Mkuu wa Shirika la Ndugu wadogo Wafransiskani ( OFM) alitaka kukumbusha katika hotuba yake


kwamba  wao ni watu ambao kiukweli wanabeba Msalaba, ambao lazima kuwapa fursa, kwa   mtazamo wa udugu na utume. Jitihada ya mwisho ilikuwa kuangazia ukarimu, upendo na unyenyekevu  kama


alivyosisitiza Kardinali Tagle kwamba ni kuwasha mshumaa na washiriki  ile  nuru katika maisha ya Kanisa na  ulimwengu. Matashi mema kwa ajili ya upyaisho wa jitihada zaidi kwa waamini


ilitoka katika  Bustani ya Botaniki ya Roma, ambapo Padre Joshtrom Isaac Kureethadam, Mratibu wa Sekta ya Ekolojia na Uumbaji ya Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya binadamu  alikuwa


ameadhimisha Misa Takatifu kwa kumbukumbu ya miaka sita tangu kuchapishwa kwa Waraka wa  Laudato si '. “Tumepokea bustani, hatuwezi kuiacha kama jangwa kwa vijana wetu na kwa maana hiyo


amesisitizai ju ya Waraka huo wa Papa wa kulinda viumbe vyote na utunzji wa mazingira nyumba yetu ya Pamoja.